Home news BEKI WA SIMBA AKUBALI YAISHE KWA YANGA…AWAKABIDHI UBINGWA MSIMU HUU..ATAJA UDHAIFU WA...

BEKI WA SIMBA AKUBALI YAISHE KWA YANGA…AWAKABIDHI UBINGWA MSIMU HUU..ATAJA UDHAIFU WA SIMBA..


BEKI wa zamani wa timu za Simba, Pilsner, Ndovu, CDA na Ashanti, Hamis Kondo ‘Cotton Juice’ anaamini Yanga itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na kumaliza ukame wa miaka minne ambayo imetawaliwa na mahasimu wao, Simba.

Yanga inaongoza ligi kwa pointi 45, nane juu ya Simba yenye pointi 37 huku kila timu ikiwa imecheza mechi 17 za ligi hiyo inayohusisha timu 16.

Kiwango kinachoonyeshwa na Yanga ambayo haijapoteza mchezo kati ya 17 iliyocheza katika ligi msimu huu, huku pia ikifikisha mechi 23 bila ya kupoteza tangu ilipochapwa 1-0 na Azam FC Aprili 25, mwaka jana, kinamfanya Kondo kuamini kwamba Wananchi wana nafasi zaidi ya kuboresha rekodi yao kwa kutwaa taji lao la 28.

Kondo ambaye jina lake la utani la ‘Cotton Juice’ ndilo alilopewa beki wa zamani ya Yanga, Kelvin Yondani ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Geita Gold, alisema: ‘Yanga lazima msimu huu ichukue ubingwa, angalia spirit yao ya kupambana timu ikiwa haijapata bao, angalia wanavyocheza kwa ajili ya timu wanapotangulia kufungwa. Simba wanakuja vizuri lakini mashindano ya Kimataifa yanawafanya wasitoe jicho ipasavyo katika ligi.”

SOMA NA HII  YANGA WAPIGA MOYO KONDE KUHUSU NGAO YA JAMII, WAELEKEZA NGUVU HUKU, UONGOZI WAFUNGUKA