Home Habari za michezo ZAA NDANIIII KABISA…SINGIDA BIG STARS YAPITA NA BEKI KISIKI WA YANGA…ISHU NZIMA...

ZAA NDANIIII KABISA…SINGIDA BIG STARS YAPITA NA BEKI KISIKI WA YANGA…ISHU NZIMA IKO HIVI…


Beki wa kushoto wa Yanga, Yassin Mustapha tayari amemalizana na Singida Big Stars (SBS) kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na muda wowote atatambulishwa.

Mustapha hakuwa na msimu mzuri Yanga na mara nyingi benchi la ufundi la Yanga lilikuwa likiwapa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza Farid Musa ama Kibwana Shomari.

Licha ya Kibwana kutumia mguu wa kulia lakini Kocha Nasreddine Nabi alikuwa akipenda kumchezesha mbavu ya kushoto ambayo hucheza Mustapha.

Mchezaji mwingine wa Yanga ambaye hucheza mbavu ya kushoto ni Brayson Raphael ambaye nae hakuwa na msimu mzuri kutokana na kuumia.

Beki huyo wa kushoto ambaye maisha yake ya Soka alianzia Dodoma katika timu ya Shelly pia amewahi kuzichezea timu za Polisi Dodoma, Stand United, Mwadui United, Coastal Union na Polisi Tanzania.

SBS itatumia uwanja wa Liti zamani Namfua kama uwanja wake wa nyumbani katika michezo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Baada ya kupanda daraja timu hiyo imebadilisha jina ikitokea Championship ilipokuwa ikiitwa DTB.

Wakala wa Mchezaji huyo, Alison Mwaliwale amesema Mustapha tayari amesaini mkataba wa miaka wiwili kuichezea timu hiyo na kinachosubiriwa ni kumtangaza.

Amesema mkataba wa Yanga na Mustapha unaisha Julai 30 mwaka huu na baada ya hapo atakuwa Mchezaji huru.

“Tumemaliza hakuna chochote anachodai Yanga na Singida bado ni kumtangaza tu ila Yassin ni mali ya Singida Big Stars kwa sababu Yanga wao wamekubali kila kitu kiwekwe wazi hata kabla ya tarehe 30,” Amesema Mwaliwale.

Wachezaji ambao tayari wamemwaga wino kuichezea timu hiyo ni mabeki, Paul Godfrey ‘Boxer’ kutokea Yanga na ‘AbdulMajid Mangalo aliyekuwa nahodha wa Biashara United.

Wengine ambao tayari wametambulishwa na SBS ni kiungo Aziz Andambwile kutokea Mbeya City na Mshambuliaji Kelvin Sabato ‘Kiduku’ aliyekuwa Mtibwa Sugar msimu ulioisha.

SOMA NA HII  CHAMA HALI SI HALI SIMBA MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU