Home Habari za michezo KUMWEMBE AMVAA MAYELE …AMPA MAKAVU LIVE…”UNATAKA KUONEKANA MFALME

KUMWEMBE AMVAA MAYELE …AMPA MAKAVU LIVE…”UNATAKA KUONEKANA MFALME

Habari za Simba leo

Kutoka kwa mchambuzi wa masuala ya soka, Edo Kumwembe ambaye amefunguka sakata la mshambuliaji wa Pyramids Fc ya Misri, Fiston Mayele kuwatupia madongo waajiri wake wa zamani, Klabu ya Yanga.

“Nadhani kuna tabia ambayo Mayele aliificha akiwa Young Africans na sasa ameifichua. Kutaka kuonekana mkubwa na mfalme.

Bahati mbaya inamuumiza pia kwamba Young Africans wanasonga mbele bila ya yeye.

Huwa inatokea unapoachana na mpenzi wako. Hautaki yamtokee mema mbele ya safari.

Lakini kuna uwezekano mkubwa Mayele anaumwa ugonjwa wa kupenda nyumbani (home sickness).

Tayari Tanzania kulishakuwa nyumbani kwake na aina ya maisha ya Tanzania yalimuingia kwelikweli. Maisha ya uwanjani, mitaani na mitandaoni.

Tanzania bado haijamtoka. Bado ipo akilini mwake. Mwili upo Misri, lakini akili ipo Tanzania.

Inawatokea wageni wengi waliowahi kuishi Tanzania.

Sio tu
wanasoka kama kina Bernard Morrison ambao tunaona kila siku wanazurura Dar es salaam ingawa wanacheza soka la kulipwa Morocco, lakini pia kwa wageni wengine.

Hata kuna mabalozi wa nchi za nje hawaishi kurudi kutembea Tanzania baada ya muda wao kuisha,” amesema Edo Kumwembe.

SOMA NA HII  A-Z JINSI YANGA WALIVYOIFANYIA 'UNDAVA' KMC JANA....MAMBO HAYAKUWA MARAHISI HIVYO...