Home Uncategorized NYOTA NANE YANGA MGUU NJE MGUU NDANI, PANGA LA ZAHERA LINAWAHUSU

NYOTA NANE YANGA MGUU NJE MGUU NDANI, PANGA LA ZAHERA LINAWAHUSU

IMEELEZWA kuwa Yanga kwa sasa hawataki utani kwani wamedhamiria kujenga kikosi imara kitakachorejesha furaha Jangwani hali iliyofanya wasajili nyota wakali.

Miongoni mwa nyota ambao wamesajiliwa ndani ya Yanga ni pamoja na Juma Balinya, Aly Ally, Maybin Kalengo,Issa Sibomana na Patrick Bigirimana inawafanya waachan na nyota wengine ndani ya kikosi hicho.

Usajili wa Yanga ambao umetikisa unampa kiburi Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ambaye ameshika hatma ya nyota wa Yanga hivyo hata ya nyota wake nane ameishikilia yeye.

Habari kutoka ndani zimeeleza kuwa wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambao wanasubiri kujua hatma yao ni pamoja na :-

Ibrahim Ajibu.

Thaban Kamusoko.

Amiss Tambwe.

Pius Buswita.

Mwinyi Haji.

Abdalah Shaibu.

Said Juma.


Mrisho Ngasa.

SOMA NA HII  BREAKING:YANGA YAMALIZANA NA MTAMBO WA MABAO