Licha ya kukiwasha wakiwa kwenye maandalizi ya msimu ujao lakini nyota wapya wa Azam wamekwamishwa na mawasiliano yao ya uwanjani kutokana na utofauti wa ligi.
Kikosi hicho juzi jumatano kilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Grand SC (1-0), ukiwa ni mchezo wa maandalizi ya msimu ujao.
Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Azam, ThabitZakaria ‘Zakazakazi’ amesema kuwa;
“hali ya huku ni nzuri natunatarajia kurudi Agosti 11 mwaka huu kurejea Dar tayari kwa ajili ya michezo ya ligi.
“Kocha ameifurahia ratiba amesema imekaa sawa kwa uwiano wa mechi za nyumbani na ugenini lakini pia muda kutoka mechi moja hadi nyingine na kama itafuatwa hivyo hivyo hadi mwisho itaifanya ligi iwe bora.
“Maingizo mapya yanafanya vizuri kujitahidi kuingia kwenye timu ila bado kuna shida ya kuelewana uwanjani lakini pia mawasiliano kwa sababu kuna wengine hawajui lugha nyingine zaidi ya kifaransa ambacho wengi hawakielewi.”