Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ametajwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Tamasha la Klabu ya Yanga la Siku ya Mwananchi.
Tamasha hilo linafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na litahitimishwa na mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya Yanga ambao ndio wenyeji dhidi ya Vipers SC kutoka nchini Uganda.
Yanga wanaitumiua siku hii maalum kutambulisha Kikosi chao cha msimu mpya na benchi la ufundi, huku zile sajili mpya kwa mara ya kwanza zikikutana na mashabiki wa timu hiyo.