Home Uncategorized TIFFAH AMRUSHA ROHO BABA YAKE

TIFFAH AMRUSHA ROHO BABA YAKE


DAR ES SALAAM: Watoto wawili ambao ni uzao wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwanamama mwenye pesa zake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ na Nillan Nasibu ‘Prince Nillan’, wamemrusha roho baba yao.

Wiki iliyopita watoto hao walijiachia na ndinga ya bei mbaya aina ya Maserati inayosemekana ni ya bwana wa sasa wa Zari yaani baba yao wa kambo aitwaye King Bae.

Wakati wakijiachia na gari hilo jipya lenye rangi nyeupe , Zari alikuwa akimuuliza Tiffah jina lake ambapo alijibu; “Tiffah.” 

Hata hivyo, hakuishia hapo bali aliendelea kumsisitiza Tiffah kutaja jina la pili kwa maana ya jina la baba yake (Diamond), lakini kama aliyeonekana kufundishwa jambo fulani, Tiffah alikuwa na kigugumiza cha kutaja jina la baba yake hadi mwisho wa zoezi hilo.

Kukosekana kwa ukaribu kati ya Diamond au Mondi na Zari kumezidi kuwaweka watoto wao mbali na baba yao kwani wanalelewa na upande mmoja wa mama nchini Afrika Kusini huku jamaa huyo akilalama kunyimwa haki ya kuwaona watoto wake hao.

Tiffah na Nillan wanaonekana kufurahia maisha wakijiachia kwenye gari hilo la mwanaume wa sasa wa Zari ambaye wenyewe wanamuita Uncle.

Wataalam wa mambo wanadai kuwa, tukio hilo la Tiffah na Nillan kujiachia kwenye gari hilo la kifahari ilikuwa ni meseji kwa Mondi ikilenga kumrusha roho na kumuonesha kuwa hata bila yeye wanafurahia maisha.

SOMA NA HII  KICHUYA, FEI TOTO WATOA TAMKO ZITO JUU YA USIMBA NA UYANGA - VIDEO