Habari za michezo

KILICHOPO NYUMA YA PAZIA ISHU YA JEZI ZA VUNJA BEI NA POLISI TANZANI….WAAMUA KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU…

admin August 21, 2022 4:24 pm


Mabosi wa Polisi Tanzania FC wamethibitisha kuachana na mdhamini wao upande utengenezaji na usambazaji wa wa jezi Kampuni ya Vunjabei.

Katika mchezo dhidi ya Yanga uliopigwa Jumanne ya wiki hii, jijini hapa na timu hiyo ilifungwa mabao 2-1, Polisi ilitumia jezi ambazo hazina nembo hata ya mdhamini mmoja.

Ulipotafutwa Uongozi wa timu hiyo kujua kulikoni, ndipo Makamu Mwenyekiti, Robert Munisi alisema walitumia jezi zisizo na nembo ya mdhamini kwani wamemaliza mkataba na Vunjabei waliokuwa wakiwavisha, ila jezi mpya zipo njiani na zitatambulishwa kwa mashabiki wao.

“Tumemaliza mkataba na Vunjabei na sasa hivi tunavalishwa na Masita, ila jezi ndio zimechelewa kufika ila tunatarajia hivi karibuni zitafika,” alisema Munisi.

Aliongeza mkataba wao na Vunja Bei ilikuwa wa mwaka mmoja na baada ya kumalizika hawajaona haja ya kuendelea nao ikabidi wasaini mkataba mpya na Masita na kuthibitisha kwamba jezi ziko njiani kutoka Uholanzi.

Kuhusu mdhamini mkuu alisema bado anabaki ni yule yule Lodhia hivyo wadau na mashabiki wao wala wasiwe na wasiwasi kila kitu kitakuwa sawa na mara hii wamepanga kuwaletea jezi zenye hadhi ya Timu ya Polisi Tanzania FC..

LIGI KUU UINGEREZA: CHELSEA WACHANA MKEKA….YAWA ‘KUBWA JINGA’ MBELE YA LEEDS…WAKUNG’UTWA KAMA NGOMA …. KUELEKEA MECHI NA LIVERPOOL KESHO….ROONEY APIGA DEBE RONALDO ASIPANGWE….KISA NI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply