Home Habari za michezo KISA SIMBA KUONGOZA LIGI MPAKA SASA….MABOSI YANGA WASHTUKIA KITU….WAITANA ‘CHAP KUPIKA JAMBO’...

KISA SIMBA KUONGOZA LIGI MPAKA SASA….MABOSI YANGA WASHTUKIA KITU….WAITANA ‘CHAP KUPIKA JAMBO’ KUBWA ZAIDI…


Mabosi wa Yanga wameshitukia kitu, haraka juzi Jumanne usiku walitarajiwa kufanya kikao na wachezaji wao na kikubwa kuwaonya kuacha kuzungumza na waamuzi na kupunguza jazba za uwanjani dhidi ya wachezaji wa timu pinzani.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kiraka wake Yannick Bangala apewe kadi ya njano baada ya kumsukuma kiungo wa Coastal Union, Mtenje Albano ambaye alimchezea rafu ya makusudi.

Kocha wa Yanga, Nasredine Nabi, alilalamikia waamuzi kwa kushindwa kuwalinda wachezaji wake kutokana na rafu za makusudi ambazo wamechezewa akiwemo Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ na Jesus Moloko ambao wanauguza majeraha.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, kutoka ndani ya Kamati ya Utendaji, amesema kuwa, kikao hicho kilipangwa kufanyika kwenye kambi yao iliyopo Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje ya Jiji la Dar.

Bosi huyo alisema kuwa lengo la kikao hicho kuwazuia wachezaji wao kuzungumza na waamuzi kwa lengo la kuepuka kadi zisizokuwa za lazima kwao wakati wakiwa na malengo makubwa ya kutetea mataji yao ya msimu uliopita.

“Viongozi wameona hizi kadi za njano wanapewa wachezaji wao zisizokuwa na ulazima, huenda zikawaletea shida baadaye kwa baadhi yao kuikosa michezo muhimu.

“Katika kuepukana na hilo, haraka viongozi wamepanga kukutana na wachezaji wao mara timu itakaporejea kambini leo (juzi Jumanne) kwa ajili ya kufanya kikao hicho kizito.

“Tunataka kuona wachezaji wetu wanaepukana na kadi za njano ambazo tumeona baadaye zitakuja kutuletea shida, kwani wachezaji wetu wanapaniwa kwa kuchezewa rafu za makusudi ambazo ni hatarishi kwa lengo la kuwapanikisha ili warudishie na kupewa kadi.

“Hilo hatutaki kuliona tena likitokea mara baada ya Bangala kuchezewa rafu ya makusudi na mchezaji wa Coastal, Mtenje alianza Sure Boy kuchezewa rafu mbaya na Inonga (Hennock) akafuatia Moloko tulipocheza dhidi ya Coastal ambaye alishindwa kurejea uwanjani baada ya rafu hiyo,” alisema bosi huyo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nasreddine Nabi, juzi alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Naomba waamuzi wawalinde wachezaji wangu, kwani wachezaji wa timu pinzani wanawachezea rafu za makusudi.

SOMA NA HII  EHEE...MASTAA BONGO WAMVULIA KOFIA 'BABU KAJU'...KAPOMBE KASHINDWA KUJIZUIA KAFUNGUKA HAYA...

“Ninaamini ipo siku wachezaji wataumizana vibaya kutokana na waamuzi kushindwa kuwalinda, nitazungumza na wachezaji wangu katika hili ili wawe makini.”