Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA LIGI KWA USHINDI…UONGOZI SIMBA WATOA MSIMAMO KUHUSU UBINGWA MSIMU...

BAADA YA KUANZA LIGI KWA USHINDI…UONGOZI SIMBA WATOA MSIMAMO KUHUSU UBINGWA MSIMU HUU…


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utapambana kuhakikisha unapata pointi nyingi mzunguko wa kwanza ili kuweza kufikia malengo ya kutwaa ubingwa.

Kwa sasa mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambaye alikiongoza kikosi cha Yanga kutwaa ubingwa bila kufungwa.

Kikosi cha Simba kinanolewa na Kocha Mkuu, Zoran Maki aliyechukua mikoba ya Pablo Franco.

Simba wao walimalaliza msimu wakiwa nafasi ya pili na kulikosa taji la ligi pia walipoteza taji la Kombe la Shirikisho pamoja na Ngao ya Jamii na mataji yote hayo yalikwenda kwa watani zao wa jadi.

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa msimu huu wanahitaji kutimiza malengo yao hivyo watapambana kufanya vizuri.

 β€œKwenye mechi ambazo tutacheza tunataka kukusanya pointi nyingi mapema hasa mzunguko wa kwanza ili kuwa imara na kufikia malengo ya kutwaa ubingwa, tunataka kuona inakuwa hivyo kabla ya mzunguko wa pili kuanza.

β€œMsimu uliopita tulianza kwa presha ya chini na tukashindwa kutetea ubingwa na kupoteza mataji ambayo tulikuwa nayo hivyo tunaamini kwamba msimu huu tutafanya vizuri,” amesema.

Mchezo wa kwanza wa ligi Simba ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold na mchezo wao ujao ni dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Agosti 20,2022 Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  ACHANA NA KIPIGO CHA YANGA...HUU HAPA UBAYA WA SIKU YA J/NNE KWA MAKOCHA WA SIMBA....