Home Habari za michezo BAADA YA KUONA TETESI ZA KUACHWA ZIMEZIDI…GADIEL MICHAEL AFANYA JAMBO SIMBA..OKRAH NAYE...

BAADA YA KUONA TETESI ZA KUACHWA ZIMEZIDI…GADIEL MICHAEL AFANYA JAMBO SIMBA..OKRAH NAYE AZIDI KUNG’ARA….


Klabu ya Simba SC Jana Agosti Mosi, 2022 imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Kholood inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia.

Magoli ya Simba yaliwekwa kimiani kupitia kwa mlinzi wa kushoto Gadiel Michael dakika ya 27 ya mchezo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa mshambuliaji Habib Kyombo.

Kiungo mshambuliaji Augustine Okrah alitupia bao la pili dakika ya 44 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Gadiel Michael.

Kipindi cha pili Simba waliendelea kuliandama goli la wapinzani wao hao lakini hata hivyo hawakufanikiwa kuongeza goli hadi dakika 90 za mchezo zinakamilika.

Mchezo huo ni wa nne wa kirafiki tangu Wekundu hao waweke kambi nchini Misri kuelekea msimu mpya wa 2022-23.

Mchezo wa awali walitoka share ya 1-1, wa pili walishinda 6-0, wa tatu waliopoteza kwa 2-0.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AONA ISIWE TABU AONGEZA BEKI MWINGINE