Home Azam FC BAADA YA KUWA MAJERUHI KWA MUDA MREFU….AZAM WAHEMA NA UJIO WA NADO….YANGA...

BAADA YA KUWA MAJERUHI KWA MUDA MREFU….AZAM WAHEMA NA UJIO WA NADO….YANGA WAJIANDAE KUZICHEZEA….


Mshambuliaji wa Azam FC Iddi Seleman ‘NADO’ huenda akaanza kuonekana tena kwenye kikosi cha klabu hiyo katika mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Young Africans.

Nado amekua nje ya Uwanja tangu Novemba 30 mwaka 2021 kufuatia majeraha ya mguu aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo siku hiyo walipoteza kwa kufungwa 1-0.

Kocha Mkuu wa Azam FC Abdihimid Moallin amethibitisha utayari wa Mshambuliaji huyo nakueleza amepona na kuingia moja kwa moja kwenye Program zake tangu timu ilipokua kambini El-Gouna nchini Misri.

“Nado yupo Fit ujue, akilaa nje kwa muda mrefu hivyo alihitaji muda wa kutosha kufanya mazoezi na kurudi kwenye ubora wake,”

“Hatukutaka kumuwahisha, lakini kwa sasa anaweza kucheza na mtamuona kwani tutakuwa tukimpa muda taratibu ili arudishe hali ya kujiamini na kushindana.” amesema Kocha huyo kutoka Marekani mwenye asili ya Somalia

Kwa upande wake Nado amesema kwa sasa yupo vizuri na amekua akifanya mazoezi na wachezaji wenzake, hivyo kama Kocha akimpa nafasi katika mchezo ujao dhidi ya Young Africans ambao utapigwa Jumanne (Septemba 06), atakuwa tayari kupambana.

“Ni muda mrefu nimekaa nje lakini kwa sasa nipo tayari, ninawaahidi tu mashabiki zangu kuwa nitaendelea nilipoishia, kama Kocha akinipa nafasi katika mchezo ujao nitapambana.” amesema Nado

Nado alilazimika kupelekwa Afrika Kusini kufanyiwa upasuaji wa (Anterior Cruciate Ligament).

SOMA NA HII  KUHUSU UNDANI WA STARS KUTOKA SARE NA ZAMBIA JANA....UKWELI USIOSEMWA HUU HAPA...