Home Habari za michezo HUYU NDIYE MAYELE….AJITENGENEZEA ‘KAREKODI KAKE’ KATAMU DHIDI YA SIMBA…KILA WAKIKUTANA LAZIMA ‘AWATOBOE...

HUYU NDIYE MAYELE….AJITENGENEZEA ‘KAREKODI KAKE’ KATAMU DHIDI YA SIMBA…KILA WAKIKUTANA LAZIMA ‘AWATOBOE TUNDU’..


Simba bado ina kidonda cha kufungwa mabao 2-1 na Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Agosti 13 lakini kana kwamba haitoshi, mabao mawili ya mshambuliaji Fiston Mayele kwenye mechi hiyo yamewaongezea kidonda kingine.

Mabao hayo mawili ya Mayele kwenye mechi ya Ngao ya Jamii yameifanya Simba kuwa miongoni mwa timu zilizofungwa idadi kubwa ya mabao kwenye mechi za kimashindano na mshambuliaji huyo nyota wa Yanga tangu alipoanza kuitumikia timu hiyo msimu uliopita.

Tangu Mayele alitua Yanga, ameifungia jumla ya mabao 22 katika mechi alizocheza za Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Ngao ya Jamii.

Katika mabao hayo Simba pekee ameifunga mabao matatu katika mechi tano alizokutana nazo, ikiwa ndio idadi kubwa ya mabao kuifunga timu moja sawa na 13.6% ya mabao yote aliyofunga straika huyo tangu alipoanza kuitumikia Yanga.

Na mabao hayo matatu aliyoifunga Simba, ameyapata katika mechi za Ngao ya Jamii mara ya kwanza ikiwa ni msimu uliopita alipopachika bao pekee na wikiendi iliyopita kufunga mawili.

Mbali na Simba, Mayele pia amefunga mabao matatu Coastal Union na Biashara United.

Kiujumla, tangu Mayele alipoanza kuitumikia Yanga, amezifunga timu 13, Simba, Polisi, KMC, Geita Gold, Biashara, Coastal, Azam, Namungo, Kagera Sugar, Mbao, Mbeya Kwanza, Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar.

Timu za Azam, Kagera na Mbeya Kwanza kila moja amezifunga mabao mawili huku zilizobakia nyingine akizifunga bao moja moja.

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUTOBOA CAF...KAZE AIBUKA NA 'KICHAMBO' KWA MASHABIKI...