Home Habari za michezo ILE SINEMA YA USAJILI WA KIUNGO MPYA MNIGERIA SIMBA IKO NAMNA HII...

ILE SINEMA YA USAJILI WA KIUNGO MPYA MNIGERIA SIMBA IKO NAMNA HII AISEE…MWENYEWE KAFUNGUKA A-Z WANAOKWAMISHA DILI..


Simba wanaendelea kimyakimya na mchakato wa kumsainisha kiungo mkabaji wa Kwara United FC ya Nigeria, Afeez Nosiru na muda wowote wiki ijayo watafanya sapraizi.

Taarifa za ndani zinadai kuwa kuna kigogo wa Simba alikuwa Nigeria na alirejea wikiendi iliyopita ambapo amefanya mazungumzo na Nosiru ila ilikuwa ngumu kuonana kwavile alizuia kuingia kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Nigeria inayojiandaa kuivaa Ghana kwenye mechi za kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN).

Nosiru alisema kwa njia ya simu kwamba mazungumzo yao yamekwenda vizuri na anawasubiri Simba kumtumia mkataba wenye mahitaji kama waliyokubaliana ili kusaini akiwa huko huko Nigeria kwani kwa sasa ni ngumu kuja Tanzania kutokana na timu ya Taifa.

Alisema kama atasaini mkataba anaweza kuja Tanzania Septemba 4 kwani wakati huu yupo katika timu ya taifa na itacheza mechi mbili za kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani dhidi ya Ghana kwa maana hiyo akiacha timu ya taifa ataonekana mtovu wa nidhamu.

“Mkataba wangu na Kwara umemalizika ila changamoto ndio hiyo timu ya taifa,maongezi yangu na Simba yamekwenda vizuri na nimepata nafasi hadi ya kuongea na mabosi kwa maana hiyo kazi imebaki kwao kukamilisha zoezi la kunisaini,”aliongeza.

“Viongozi hao wameniambia usajili wa ndani unafungwa Agosti 31 kwa maana hiyo kazi ni kwao kama tutamalizana kabla ya siku hiyo binafsi nipo tayari,isingekuwa timu ya taifa pengine wakati huu ningekuwa Tanzania,”aliongeza.

Katika hatua nyingine Simba iliulizia uwezekano wa kumpata kiungo mkabaji wa Rivers United, Morice Chukwu (27) ila wanaweza kukutana na changamoto ya mkataba aliokuwa nao.

Chukwa alisema kuwa aliongea na mmoja wa viongozi Simba na kuwaeleza bado anamkataba wa miezi sita na Rivers ambao viongozi wake wameweka ngumu kumuachia kutokana na kukosa mbadala wake.

“Nipo kambi ya Nigeria najaribu kuwaomba zaidi viongozi wa Rivers kama watakubali kuniachia niende Simba kwani ni moja ya timu kubwa Afrika kwa sasa ila ikishindikana haina jinsi,”alisema. Kama Simba itasajili mmoja wa hao kuna uwezekano mkubwa Victor Akpan akarejeshwa kwa mkopo Coastal Union.

SOMA NA HII  KISUBI AVUNJA UKIMYA SIMBA...ATOA KAULI NZITO AKISEPA KUJIUNGA NA MTIBWA...ADAI UTU WAKE....