Home Habari za michezo KIPIGO KUTOKA KWA VIPERS CHAMSHTUA NABI…ASINGIZIA KAMBI NA MAZOEZI…

KIPIGO KUTOKA KWA VIPERS CHAMSHTUA NABI…ASINGIZIA KAMBI NA MAZOEZI…


Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa baada ya kupoteza kwa mabao 2-0, dhidi ya Vipers, Jumamosi iliyopita Agosti 6, 2022, imemsaidia kujua mapungufu ya kikosi chake.

Yanga ilicheza na Vipers kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi katika kilele cha siku ya Mwnanchi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Nabi alisema kuwa mapungufu ambayo yamejitokeza kwenye mchezo huo yametokana na uchache wa siku walizokaa kambini lakini anarudi kwenye uwanja wa mazoezi kuyafanyia kazi.

“Hata mimi nilitamani kupata ushindi kwenye mechi hii lakini niseme tu mashabiki wasiwe na hofu,”

“Baadhi ya wachezaji wamefanya makosa lakini ilitokana na ukweli kwamba hawakufanya mazoezi kwa muda na niliwaongezea siku za kupumzika kwa sababu msimu uliopita ulikuwa mgumu sana,”.

“Zaidi kwangu ilikuwa ni mechi ya kirafiki na lengo lilikuwa ni kuangalia kile nilichofanyia kazi kambini.”alisema Nabi.

Akizungumza baada ya mchezo kocha mkuu wa Vipers, Roberto Oliviera, alisema kuwa anawapa hongera Yanga kwa sherehe kwani mabingwa hao ni timu yenye wachezaji wazuri.

“Tunaanza maandalizi hayo kwa mchezo wa leo (juzi) tumeshinda mabao mawili nimefurahishwa na kiwango cha wachezaji wangu kipindi cha pili nilibadili mfumo wa uchezaji ili kuangalia ubora wa wachezaji wangu,”

SOMA NA HII  IMEVUJA!! MABOSI SIMBA WAMWAGA MANOTI...WAIFUNGIA KAZI YANGA