Home Habari za michezo KUDADEKI….JEZI MPYA YANGA ZAWEKA REKODI NYINGINE TZ….MASHABIKI WAZIGOMBEA KAMA NJUGU…MZIGO WOTE WAISHA…

KUDADEKI….JEZI MPYA YANGA ZAWEKA REKODI NYINGINE TZ….MASHABIKI WAZIGOMBEA KAMA NJUGU…MZIGO WOTE WAISHA…


Saa chache tangu Yanga izindue jezi mpya za msimu wa 2022-2023 juzi usiku, huko mtaani zimekuwa gumzo kwa mwonekano wake, huku zikigombewa kama njugu na mashabiki wa klabu hiyo na mpaka juzi jioni zaidi ya jezi 70,000 za mzigo wa kwanza zilikuwa zimeisha.

Yanga ilizindua jezi aina tatu zikiwamo za njano kwa mechi za ugenini zenye michoro flani inayonasibishwa na matawi ya klabu hiyo, za nyumbani zikiwa na rangi ya kijana zenye michoro ya majengo na alama mbalimbali zinazotambulisha vivutio vya miji iliyopo nchini na jezi nyeusi ziliwadatisha mashabiki na kuzinunua kwa wingi zenye saini na majina ya nyota wa zamani.

Taarifa kutoka mitaani kuhusu namna mapokezi ya uzi mpya yalivyokuwa na kubaini nyeusi zikinunuliwa na kumalizika kwenye duka lililopo makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, huku baadhi ya mashabiki wakilalamika kutokuwa na namba mgongoni.

Jezi hizo zinazouzwa kwa Sh35,000 kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita zilikuwa zikigombewa na mashabiki waliojazana klabu, huku nyeusi zikiongozwa kununuliwa zikifuatiwa na za njano, huku za kijani ambazo mitandaoni zilikuwa gumzo zinunuliwa na kuisha.

Mmoja wa mashabiki wa Yanga aliyejitambulisha kwa jina la Mohammed, akiwa na jezi nyeusi, alisema uongozi ungeziweka namba ingekuwa tamu kwani watu wangezinunua kulingana na hitaji la namba za wachezaji wa klabu hiyo.

SOMA NA HII  PANGA LA YANGA KUPITA NA MASTAA HAWA...INJINIA HERSI ATAJA MFUMO WATAKAOTUMIA...