Home Uncategorized JKT TANZANIA YAKWAMA KUSEPA NA POINTI TATU NDANI YA DAKIKA 450

JKT TANZANIA YAKWAMA KUSEPA NA POINTI TATU NDANI YA DAKIKA 450


 KIKOSI cha JKT Tanzania kipo kwenye wakati mgumu kwa sasa baada ya kushinda mbele ya Mwadui FC kwa mabao 6-1 kimekwama kupata ushindi kwenye mechi zake tano ambazo ni dakika 450 mfululizo zaidi ya kuambulia sare mbili na kupata vipigo mechi tatu.

Chini ya Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed, ‘Bares’ kikosi kimecheza mechi 13, kimeshinda mechi mbili huku kikipoteza mechi saba na kutoa sare nne kipo nafasi ya 16 na pointi zake 10 kibindoni.

Mara ya mwisho kushindi ilikuwa ni Oktoba 25, mbele ya Mwadui 1-6 JKT Tanzania Uwanja wa Mwadui Complex baada ya hapo mechi zake zinazofuata mambo yamekuwa magumu.


Adam Adam mshambuliaji namba moja wa kikosi cha JKT Tanzania aliweka rekodi ya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 ana jumla ya mabao sita.

Mambo yalikuwa namna hii baada ya kupata ushindi wake wa pili mbele ya Mwadui:-Oktoba 30, JKT Tanzania 1-1 Azam FC, Uwanja wa Azam Complex. Novemba 4, Namungo 2-2 JKT Tanzania, Uwanja wa Majaliwa. Novemba 21, JKT Tanzania 0-2 Gwambina, Uwanja wa Samora.

Novemba 24, JKT Tanzania 0-1 Mbeya City, Uwanja wa Samora.Novemba 28, Yanga 1-0 JKT Tanzania, Uwanja wa Mkapa.

Bares amesema kuwa vijana wake wanacheza kwa juhudi ila wanakosa matokeo ndani ya uwanja jambo ambalo anaamini litafika kikomo hivi karibuni.

 

SOMA NA HII  TAARIFA KUHUSU NAFASI YA MWENYEKITI WA YANGA KUDAIWA KUJIUZULU