Home Geita Gold FC KUELEKEA MECHI YAKE YA KWANZA YA LIGI DHIDI YA SIMBA…MINZIRO NA...

KUELEKEA MECHI YAKE YA KWANZA YA LIGI DHIDI YA SIMBA…MINZIRO NA GEITA YAKE WAJIVUNIA USAJILI WA KIMYA KIMYA…


KOCHA Mkuu wa Geita Gold, Fred Minziro amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa ukimya wao kwenye suala la usajili ni mbinu yao ambayo wanaamini itawashangaza wengi kwenye mchezo wao na Simba.

Geita itaanzia ugenini Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Agosti 17 mwaka huu kuikabiri Simba ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza , Minziro alisema kwa asilimia kubwa ripoti aliyoipeleka kwa viongozi imefanyiwa kazi kilichobaki kwake ni kukiandaa kikosi cha ushindani wa ndani na michuano ya kimataifa ambao wanashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Alisema anaamini ujio mpya wa nyota hao utaimarisha kikosi chake ili kiweze kuendelea pale walipoishia huku akitaja mchezo wao wa kwanza ndio utatoa picha halali ya kikosi chao kuelekea msimu mpya.

“Niliomba kuongezewa wachezaji nane kwa asilimia kubwa hili limefanyika na bado dirisha linaendelea tunakutana na Simba ubora wa kikosi nilichonacho natarajia mchezo mzuri na wa ushindani,” alisema na kuongeza;

“Nawaheshimu wapinzani wangu, najua ni timu bora na kubwa Tanzania lakini sisi pia tuna kikosi imara na shindani tunataka matokeo mazuri ili kuwa na mwendelezo mzuri kwenyye ligi na kutupa nguvu kuelekea mashindano ya kimataifa,” alisema Minziro.

Aliongeza anafahamu msimu ujao utakuwa na ushindani hivyo amekiandaa kikosi chake kwa kufanya marekebisho sehemu zilizokuwa na mapungufu msimu uliopita ili kuonyesha ushindani.

Geita Gold ilimaliza msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya nne na imekata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Hadi sasa Geita imewatangaza nyota watatu waliowasajili ambao ni Shown Oduro, Miraji Athmani na Yahya Mbegu.

SOMA NA HII  VIDEO: NYOTA KAIZER CHIEFS, SIMBA ITAWEZA KUFIKIA MAFANIKIO