Home Uncategorized DODOMA JIJI BANA, WATEMBEZA 5G, WAOMBA RADHI KWA MASHABIKI

DODOMA JIJI BANA, WATEMBEZA 5G, WAOMBA RADHI KWA MASHABIKI


 LICHA ya kupata ushindi wa mabao 5-1 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Hollywood FC uliochezwa jana, Januari 6, Uwanja wa Jamhuri Dodoma, uongozi wa timu hiyo umeomba radhi kwa ushindi walioupata.


Ushindi huo unaifanya Dodoma Jiji yenye maskani yake Dodoma kutinga hatua ya 32 bora ya Kombe la Azam Sports Federation ambalo lipo mikononi mwa Simba.


Mabao hayo yalipachikwa na Justin ambaye alipachika mabao mawili dakika ya 2 na 27, Kanyora alipachika bao moja dakika ya 39 na mawili mengine yalipachikwa na Hamis Mcha dakika ya 46 na 50.


Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fortunas Johnson amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kufikia malengo ambayo wamejiwekea na kuomba sapoti kwa mashabiki.

“Tunawashukuru mashabiki kwa sapoti kubwa ambayo wanatupa hiyo ni furaha kwetu na malengo yetu ni kuona kwamba tunapiga hatua kubwa zaidi ya hapa,” .


Kupitia Ukurasa wao rasmi wa Istagram Dodoma Jiji waliandika namna hii:”Tunaomba radhi mashabiki wetu kwa ushindi mwembamba siku ya leo, kikubwa tumefuzu hatua inayofuata,”.

SOMA NA HII  MGUNDA WA COASTAL UNION ATAJA IDADI YA WACHEZAJI ATAKAOWASAJILI