Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA KURUDI TENA BONGO….NIYONZIMA AANIKA JINSI VIGOGO WA SOKA BONGO...

KUHUSU ISHU YA KURUDI TENA BONGO….NIYONZIMA AANIKA JINSI VIGOGO WA SOKA BONGO WANAVYOMPAPATIKIA…


Kiungo aliyewahi kutamba na Yanga pamoja na Simba, Haruna Niyonzima amekiri kufuatwa na timu za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo zimetaka huduma yake, lakini Mnyarwanda huyo akazichomolea.

Timu ambazo zimekuwa zikihusishwa kusakata ni pamoja na Singida Big Stars na Geita Gold, ambapo Niyonzima amesema;

“Ni kweli timu zaidi ya mbili zilinitafuta zikitaka huduma yangu lakini hatukuweza kufikia makubaliano kutokana na maslahi binafsi.

“Ujue mpira ndio unaendesha maisha na faimilia yangu mali nilizonazo zote zimetokana na mpira hivyo lazima niuheshimu na kuwa na mipaka ya maslahi nadhani hiyo ndio sababu kuu ya dili hizo kutokamilika,”

Niyonzima ameongeza kuwa hajachuja kiwango kutokana na nidhamu, malengo na kujituma kwake mazoezini na uwanjani. Sasa anakipiga timu ya AS Kigali ya Rwanda, pia ni nahodha wa Rwanda (Amavubi)

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JJUMATANO