Home Habari za michezo MBEYA CITY NAO WAONYESHA JEURI YA PESA…WAMPA KAZI KOCHA WA TIMU YA...

MBEYA CITY NAO WAONYESHA JEURI YA PESA…WAMPA KAZI KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA UGANDA…


Baada ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar juzi, leo Mbeya City imeendelea na mazoezi huku ikishuhudiwa Kocha mpya wa timu hiyo, Abdallah Mubiru raia wa Uganda akifuatilia program yao jukwaani.

City ilikuwa na mchezo wa kujipima nguvu na Mtibwa Sugar huko Turiani Morogoro na kushinda 3-1 ikiwa ni mechi ya kwanza kwao kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu 2022/23 unaoanza Agosti 17 mwaka huu.

Katika mazoezi ya leo ambayo hayakuchukua zaidi ya saa moja, yalilenga kuweka mwili fiti kabla ya kesho kuendelea na program rasmi.

Mubiru akiwa kwenye gari alionekana akifuatilia matizi ya nyota wake mwanzo mwisho.

Mubiru aliyewahi kuzinoa Vipers, KCCA na timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ anatarajiwa kukabidhiwa mikoba ya timu hiyo iliyoachwa na mwenzake Mathias Lule aliyetimkia Singida Big Stars na atatamburishwa muda wowote kuanzia kesho kwa wachezaji.

Habari za ndani zimeeleza kuwa bado Kocha huyo hajamalizana na mabosi wake moja kwa moja isipokuwa wapo katika mazungumzo ya mwisho ili kuanza rasmi kazi ya kuinoa timu hiyo msimu ujao.

Hata hivyo, katika mazoezi hayo wachezaji wote wamewasili akiwamo sura mpya, Kiungo Awadh Juma kutoka Dodoma Jiji, huku Naasoro Machezo naye akitarajia kutua siku yoyote kuanzia leo.

SOMA NA HII  SHINDA MAOKOTO NA FISHTASTIC KASINO YA UVUVI BAHARINI...