Home Habari za michezo MCHAMBUZI WA MICHEZO AULA KMC….ATEULIWA KUWA MTENDAJI MKUU….ARITHI MIKOBA YA MENEJA WA...

MCHAMBUZI WA MICHEZO AULA KMC….ATEULIWA KUWA MTENDAJI MKUU….ARITHI MIKOBA YA MENEJA WA YANGA….


Baada ya kuondoka kwa Walter Harrison, Uongozi wa klabu ya KMC umemtangaza Daniel Mwakasungula kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo.

Walter ambaye aliiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa aliondoka hivi karibuni kwenye klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Yanga.

Majukumu aliyonayo Walter ndani ya klabu ya Yanga kwa sasa ni kuwa Meneja wa kikosi hicho ambacho jumamosi kilitwaa Ngao ya jamii baada ya kuifunga Simba kwa mabao 2-1.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka KMC zimeeleza kuwa “Bodi ya klabu ya KMC imemteua Ndugu, Daniel Mwakasungula kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu”.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa KMC, Mwakasungula alikuwa mchambuzi wa Michezo kwenye Redio ya Times FM.

Kikosi cha KMC kinatarajia kushuka dimbani Agosti 17, mwaka huu kumenyana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

SOMA NA HII  ISHU YA CHAMA KUMALIZANA NA YANGA...MANARA AFUNGUKA HAYA TENA..