Home Habari za michezo PAMOJA NA HALI DUNI WALIYONAYO…ZALAN FC WAAPA KUFA NA YANGA CAF…KOCHA WAO...

PAMOJA NA HALI DUNI WALIYONAYO…ZALAN FC WAAPA KUFA NA YANGA CAF…KOCHA WAO AFUNGUKA KWA UCHUNGU…


Baada ya kutambulishwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Zalan FC, Baping Alliab, ameanza kuchonga kwa kusema ataanza kufanya vema katika michuano ya kimataifa kwa kuhakikisha anaipeleka mbali timu hiyo na si kuishia hatua ya awali.

Zalan FC watakipiga na Yanga katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, michuano inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Septemba 9 nchini Sudan Kusini, kisha marudiano Septemba 16, mwaka huu jijini Dar.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Zalan FC, kocha huyo alisema: “Tunatakiwa kuhakikisha hatuondolewi mapema katika michuano hii ya kimataifa, tayari nimeshazungumza na viongozi, mipango yao ni kuona timu inafika mbali na sio kutolewa mapema.

“Malengo yao kama viongozi yanatakiwa kuwa katika akili zetu pia japo najua michuano hiyo mikubwa Afrika ni migumu kwa kuwa tutakutana na timu ngumu, lakini hatutakiwi kukubali kushindwa.”

SOMA NA HII  KIGOGO WA SOKA AFRIKA AVUNJA UKIMYA..."YANGA INA NGUVU KUBWA SANA