Home Habari za michezo SAKATA LA DILUNGA KUTEMWA SIMBA…OSCAR OSCAR AIBUKA NA HILI KUHUSU UTENDAJI WA...

SAKATA LA DILUNGA KUTEMWA SIMBA…OSCAR OSCAR AIBUKA NA HILI KUHUSU UTENDAJI WA BARBARA…”WANAMUONEA BURE”…

 


Baada ya Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally kuweka wazi kuwa Klabu ya Simba imeachana na Kiungo wake Mshambuliaji Hassan Dilunga “HD” na kuamua kutomuongezea mkataba.

Wadau wa Soka wameilalamikia Klabu ya Simba kwa kitendo hicho hasa ikizingatiwa mchezaji huyo ambae ni majeruhi kwa sasa mara ya mwisho kuonekana uwanjani alionekana na jezi ya Simba.

Majeraha anayoendelea kuyauguza Dilunga pia ameyapata wakati anaitumika Klabu ya Simba SC.

Maneno mengi ya wapenda Soka yameeelkezwa kwa Mtendaji wa Simba Barbara Gonzalez kwa kumueleza kuwa kitendo hiko ni kitendo cha Kinyama.

Sasa mchambuzi mahiri wa Soka nchini Oscar Oscar ameibuka na kumkingia kifua CEO huyo.

Oscar Oscar anasema kuwa;

wanaomsema vibaya Barbara kuhusu maamuzi ya Simba kuachana na Hassan Dilunga na mengine pia wanakosea.

Anasema maamuzi yote anayoyafanya yanatokana na bodi ya wakurugenzi ambao wanaamua malengo ya klabu na sio malengo yake binafsi.

Oscar anaongeza kuwa, Simba kama klabu imefanya kwa nafasi yake kumuhudumia mchezaji toka alipokuwa majeruhi ndani ya kipindi cha mkataba na kwa kawaida inaposalia miezi sita kwa mkataba kumalizika milango inakuwa wazi kwa mchezaji kuamua iwapo anahitaji kutafuta changamoto nyingine.

Anatoa mfano wa Arsenal ambao walimuhudumia Santiago Cazorla na baadae kuamua kuachana nae.

Hata hivyo katika maelezo yake Ahmed Ally alisema mpaka sasa Simba inawajibika na matibabu ya mchezaji huyo licha ya kuachana nae.

SOMA NA HII  SIMBA WANAHESABU NDEFU KIMATAIFA