Home Habari za michezo WAKATI AKITUMIKIA KIFUNGO CHAKE…MANARA ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA HILI JIPYA KWA TFF…ATAJA ISHU...

WAKATI AKITUMIKIA KIFUNGO CHAKE…MANARA ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA HILI JIPYA KWA TFF…ATAJA ISHU YA KUBAKA..


Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, haji Manara ambaye amefungiwa na TFF kujihusisha na masuala ya Soka kwa muda wa miaka miwili.

Anatitirika; “Nafahamu Watu wengi wamefungiwa au kusimamishwa kujihusisha na Mpira lakini hawabanwi kama mimi.

Nazuiwa hadi kuja Uwanjani kutazama mechi yoyote ya Soka,Wanahoji hadi nikipost Instagram, Lau wangekuwa na Mamlaka za TCRA au ndio wangekuwa Owners wa Instagram wangehakikisha Account hii imeshajifia.

Imagine, Sasa hivi wameenda mbali zaidi , Wanahoji Kwa nini nilisafiri kwenda Arusha Wakati Yanga inacheza kule? Hapo ndio sikwenda hata uwanjani kutazama mechi zetu, Wanadai eti siruhusiwi kusafiri Mji ambao Yanga wapo, Wanachomaanisha Champion akicheza Dar inabidi nihame Mji sio?

Mbaya zaidi ni kujaribu hata kunibana katika Shughuli zangu binafsi ikiwemo biashara zangu za Matangazo, shughuli zangu hizi zinazuia nini kifungo chao? Kwa hiyo nisile wala kunywa? Kimsingi hapa wananizuia hata kulipa kodi kutokana na Mapato yangu.

Utadhani labda nimeua au nimebaka Watoto wadogo, kumbe ni makosa hewa yaliyokosa any prove hata kwao wenyewe.

Inanifadhaisha mno na ndio maana awali niligoma hata kutoa neno la Rambi Rambi leo Msibani, nikiogopa kuonekana najihusisha na mambo ya Mpira, Maana Marehemu Hadija alikufa akienda Mpirani Arusha,tena akiwa Shabiki wa Yanga.

Vipi kwa wenzangu iwe ruksa ila kwangu iwe hata nanyimwa kuuziwa tiketi za kwenda Qatar, kutazama World Cup tena kwa gharama zangu mwenyewe ?

Mpira huu huu au kuna mengine? Siku c nyingi ntaulizwa kwa nini unapumua Wakati umefungiwa? Si bora mninyonge tu ili mpumzike.

Hivi Basata wanapofungia Wasanii hukatazwa hata kwenda Disco au Dansini?

Okay, Once again Poleni sana Wafiwa na Tunaendelea kuwaombea Subira kwa Mwenyezi Mungu Insha’Allah ????????????????

Nb:: Usiniulize Kama nimeshakata Rufaa,Yes kitambo sana lakini Siamini hata kama itasikilizwa”.

HAJI MANARA.

SOMA NA HII  FAMILIA WAWEKA WAZI SABABU YA KIFO CHA MWL KASHASHA..ALILAZWA KWA WIKI MBILI