Home Habari za michezo WALIOPIGWA PANGA SIMBA HAWA HAPA…BOCCO, NTIBAZONKIZA MHHH…..

WALIOPIGWA PANGA SIMBA HAWA HAPA…BOCCO, NTIBAZONKIZA MHHH…..

Habari za Simba leo

UONGOZI wa Simba umeatangaza kuachana na wachezaji wazawa wanne Simba imetangaza kuachana na Shaban Chilunda, Nassor Kapama, Jimmyson Mwanuke na Mohammed Mussa katika kipindi cha dirisha dogo la usajili lililifungwa jana (Jumatano, Januari 15, mwaka huu).

Simba wameachana na wachezaji hao kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha wekundu hao kinachoongozwa na kocha Abdelhak Benchikha.

Katika majina hayo kuna baadhi ya wachezaji wametolewa kwa akiwemo Kapama ambaye anaenda kuitumikia wakata miwa wa Manungu, Mtibwa Sugar.

Taarifa za iliyotolewa kupitia mitandao ya Simba kuwa wameachana na nyota hao na kuwatakia maisha mazuri waendako katika majukumu yao mapya.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema wamefanya maamuzi magumu kuachana na nyota hao kwa sababu ya ushindani wa namba ulipo ndani ya kikosi cha timu.

Amesema mashindano ya kombe la Mapinduzi imempa picha kocha Benchikha na kuona wachezaji ambao atakuwa nao katika kipindi hiki za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, FA na Ligi ya Mabingwa ambayo wanaenda kucheza na Asec Mimosas Februari 24, mwaka huu.

“Kila jambo kuhusu usajaili na kuondoka kwa baadhi ya wachezaji ni mapendekezo ya benchi la ufundi, hii ni baada ya kupata muda mzuri wa kukaa na timu na kuwapa nafasi kila mchezaji na kuona uwezo wake.

Walioacha haina maana wabaya ila kulingana na ushindani uliopo ndani ya kikosi na malengo ambayo tumejiwekea kuelekea mzunguko wa pili w ligi, FA na michuano ya kimataifa lazima tufanye maboresho kidogo,” amesema Meneja huyo.

SOMA NA HII  UBORA WA YANGA MSIMU UWE KENGELE YA HATARI KWA SIMBA...WAACHE UBAHILI WA KUSAJILI...LA SIVYO JAHAZI LITAZAMA KABISA..