Home Habari za michezo WAKATI HATA UHAKIKA WA KUPATA NAFASI HAUPO…NKANE AIBUKA NA HAYA MAPYA KWA...

WAKATI HATA UHAKIKA WA KUPATA NAFASI HAUPO…NKANE AIBUKA NA HAYA MAPYA KWA YANGA…’AJIPALILIA MOTO JIKONI’…


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Denis Nkane ‘Wonder Kid’ amesema kuwa maandalizi ya kikosi chao kuelekea msimu mpya ni mazuri hivyo wana uhakika mpaka ligi inaanza kikosi chote kitakuwa kimekaa mguu sawa kwa ajili ya kutetea mataji yao.

Nkane amesema kuwa kwa usajili uliofanywa na mabosi wa Yanga, wana uhakika watatetea mataji yao yote matatu (Ngao ya Jamii, Shirikisho na Ligi Kuu) ikiwezekana na kuongeza mengine yatakayokuja.

“Najisikia furaha kuwa sehemu ya timu kikosi cha Yanga ambayo ni timu kubwa nchini Tanzania, timu inayoshiriki mashindano makubwa ya kimataifa, lakini ni timu ambayio ina uhakika wa kuchukua makombe yote.

“Maandalizi ya msimu mpya ni mazuri na tumeyaanza vizuri, licha ya kutokuanza na wenzangu lakini tulipewa program maalum ambayo kila mmoja alikuwa akifanya mapumzikoni. Kwa hiyo maandalizi haya yatatuweka sawa kufanya vizuri kimataifa na tunakwenda kutetea vikombe vyote vitatu.

“Ni furaha sana kwangu kuona leo nacheza na Gael Bigirimana, ni mtu mwenye cv kubwa, amecheza timu kubwa, anaujua mpira.

“Ukimzungumzia Aziz Ki ni mtu ambaye amecheza mpira level za juu, kwa hiyo kuwa nao kwenye kikosi kwangu mimi ni furaha na ninajifunza mengi kutoka kwao ukizingatia mimi ni kijana na nina malengo ya kufika mbali,” amesema Nkane.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AMKINGIA KIFUA NGOMA