Home Habari za michezo WIKI KADHAA TOKA MECHI YA NGAO YA JAMII KUPITA…MAYELE AFUNGUKA MAPYA KUHUSU...

WIKI KADHAA TOKA MECHI YA NGAO YA JAMII KUPITA…MAYELE AFUNGUKA MAPYA KUHUSU BIFU LAKE NA INONGA…”ALINIUDHI’


Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele amezungumzia tukio la mchezaji mwenzake raia wa Congo DR anayekipiga kunako Klabu ya Simba, Henock Inonga ambaye alimsindikiza nje ya uwanja katika mechi ya ambayo walitoka sare.

Akizungumza na Haji Manara, Mayele amesema Inonga alifanya utoto msimu uliopita kwa kumsindikiza nje kwa dhihaka akiomba aletewe mwingine aingie.

Amezungumza haya alipoulizwa kuhusu yeye na Bangala kuonesha ishara ya kumchapa Inonga baada ya mchezo wa Ngao.

“Inonga ni ndugu yangu, ni rafiki yangu na tunatoka taifa moja na tunacheza wote timu ya taifa, tukio alilonifanyia msimu uliopita kiukweli liliniudhi.

“Mimi kama mimi siwezi kufanya mambo kama yale, nilisema nikilipa deni lazima na mimi nimchape,” Fiston Mayele.

Aidha, Mayele amekiri aliumizwa sana kwa kukosa kiatu cha ufangaji bora wa ligi kuu Tanzania bara kwani alistahili kiatu hicho.

Mayele ameendelea kusema;

Baadhi ya magoli yake ambayo hayakuwa na shida yoyote yalikataliwa likiwemo la Mchezo wa mwisho dhidi ya Mtibwa Sugar.

Amesisitiza kuwa hajakata tamaa, na malengo yake msimu huu ni kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara.

SOMA NA HII  HII HAPA NDIO MITEGO MIWILI YA YANGA