Home Habari za michezo ZA UHAKIKA HIZI….BAADA YA KUONA HAPATI NAMBA…KIPA SIMBA AVUNJA MKATABA…AKIMBILIA POLISI KUWEKA...

ZA UHAKIKA HIZI….BAADA YA KUONA HAPATI NAMBA…KIPA SIMBA AVUNJA MKATABA…AKIMBILIA POLISI KUWEKA MAMBO SAWA..


Uongozi wa Polisi Tanzania umekamilisha usajili wa aliyekuwa kipa wa Simba, Jeremiah Kisubi kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuziba pengo la Metacha Mnata aliyetimkia Singida Big Stars.

Kisubi amejiunga na Polisi Tanzania akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Simba ambao walimsajili kwa miaka mitatu akitokea Tanzania Prisons.

Akizungumza Makamu Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, Robert Munisi, alisema ni kweli wamemalizana na kipa huyo akiwa huru wanatarajia mazuri kutoka kwake kutokana na uzoefu mkubwa alionao kwenye ligi.

“Ujio wake utakuwa na tija kwenye kikosi chetu baada ya kuondoka kwa Metacha tulikuwa na Kelvin Igendelezi ambaye hana uzoefu mkubwa ujio wa Kisubi utaongeza chachu ya ushindani,” alisema Munisi na kuongeza;

“Tunahitaji kuwa na kikosi bora na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye kila nafasi uwepo wake utatoa changamoto kwa aliyemkuta na tunaamini ataongeza kitu kwenye timu yetu.

Wakati huohuo Kisubi alisema yeye ni mali ya Polisi Tanzania kwa sasa baada ya makubaliano ya pande mbili kati yake na Simba kuhusu kuvunja mkataba kukamilika.

“Ni kweli nilikuwa na mkataba wa miaka mitatu na Simba ambao walinitoa kwa mkopo Mtibwa Sugar baada ya kumaliza mkataba wa mkopo nimekaa mezani na uongozi wa Simba na kukubaliana kuvunja mkataba ili niwe huru baada ya hilo kukamilika ndipo nilipoamua kumalizana na Polisi Tanzania nimejifunga huko miaka miwili.” alisema.

SOMA NA HII  NI MWENDO WA NEEMA JUU YA NEEMA...WAZIRI MKUU NAYE ATOA NENO KWA YANGA...