Home Habari za michezo NI MWENDO WA NEEMA JUU YA NEEMA…WAZIRI MKUU NAYE ATOA NENO KWA...

NI MWENDO WA NEEMA JUU YA NEEMA…WAZIRI MKUU NAYE ATOA NENO KWA YANGA…

Habari za Yanga leo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaipongeza klabu ya Yanga kwa hatua ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika akisema ni kanuni pekee imewanyima Kombe hilo lakini waliupiga mwingi.

Majaliwa ameyasema hayo baada ya kupiga simu kituo cha Radio Cha Wasafi wakati Rais wa Yanga Hersi Said akifanyiwa mahojiano asubuhi hii akisema amefurahishwa na hatua kubwa ya Yanga.

Amesema katika mchezo huo wa fainali ya pili uliopogwa juzi nchini Algeria Yanga ilicheza soka kubwa na kufanikiwa kushinda lakini kanuni pekee ndio imewanyima Kombe

“Nawapongeza sana Yanga hakika mlicheza mpira mkubwa na mkafanikiwa kushinda kwa maana kubwa sisi ndio washindi ni kanuni pekee ndio imewanyima kombe lakini tuliwazidi Waalgeria,”amesema Majaliwa

“Nawapongeza sana viongozi mlifanya kazi kubwa, nawapongeza benchi la ufundi liliandaa timu vizuri lakini pia wachezaji walipambana sana uwanjani.

Aidha Majaliwa amewataka Yanga kuendelea na morali hiyo ya kutamani kushinda makombe zaidi kama ambavyo wanavyofanya katika kila msimu.

SOMA NA HII  ASIKWAMBIE MTU BANA...HIZI HAPA SABABU ZA SIMBA KUMCHAGUA PABLO...WACHEZAJI WAITWA FASTA...