Home Habari za michezo KOMBE JIPYA LIGI KUU HILI HAPA….KUHUSU KUKABIDHIWA KWA YANGA AU LAH..UKWELI HUU...

KOMBE JIPYA LIGI KUU HILI HAPA….KUHUSU KUKABIDHIWA KWA YANGA AU LAH..UKWELI HUU HAPA..

Kombe Jipya la NBC

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetambulisha Kikombe kipya cha Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, leo Juni 7, 2023 katika ukumbi wa makao makuu ya NBC uliopo Posta ya zamani, Dar es Salaam.

Haya yanajiri baada ya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa mpira wa miguu kuhusu muonekano wa Kikombe kilichotangazwa msimu uliopita ambapo iliamuliwa kwa pamoja kufanyika maboresho katika eneo hilo muhimu ili kuendana na hadhi na kiwango cha Ligi yetu inayoendelea kujizolea umaarufu na mvuto kila siku barani Afrika na duniani.

Kikombe hicho kitakabidhiwa kwa Bingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023, klabu ya Young Africans Juni 9, 2023 baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons na kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Yanga imetwaa taji hilo mara ya pili mfululizo ikiwa ni msimu wa 2021/22 na msimu huu pia wa 2022/23 lipo mikononi mwa Yanga.

SOMA NA HII  UKWELI MCHUNGU....JEZI ZILIZOKAMATWA SIO FEKI...NI MICHEZO YA KARIKAOO..SANDALAND KAZIDIWA...