Home Habari za michezo AHMED ALLY ATAMBA KUHUSU UBINGWA, KUHUSU SOKA BIRIANI AWAPA NENO HILI MASHABIKI

AHMED ALLY ATAMBA KUHUSU UBINGWA, KUHUSU SOKA BIRIANI AWAPA NENO HILI MASHABIKI

Habari za Simba SC

Ahmed Ally ambaye Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, amesema ili wajihakikishie nafasi kubwa ya kuuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, hawataruhusu sare yoyote katika michezo inayofuatia.

Hiyo ni baada ya juzi kupata ushindi wa tano mfululizo katika michezo ya ligi msimu huu na kuongoza msimamo wakifikisha pointi 15. Simba ilipata ushindi wa mabao 1-2 ugenini dhidi ya Singida Fountain Gate, mchezo uliochezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Akizungumza nasi, Ally alisema wanachoangalia hivi sasa ni pointi tatu ili wafanikishe malengo yao ya msimu huu kwa kubeba ubingwa, huku akiahidi kuendelea na mwendelezo wa ushindi katika michezo ijayo.

Ally alisema msimu huu wamekuja na kauli mbiu ambayo kwao sare yoyote haramu, ni bora kwao kupata ushindi kiduchu wa bao moja, lakini pointi tatu lazima.

Aliongeza kuwa, uongozi unafurahishwa na mabadiliko ya soka ambalo wachezaji wamelicheza dhidi ya Singida, lilotosha kuwapa burudani mashabiki wa timu hiyo.

“Hatutaki kutoka mchezoni, kikubwa sisi Simba tunataka kuona timu yetu ikiendeleza ushindi katika kila mchezo uliokuwepo mbele yetu ili tubaki kileleni kwenye msimamo hadi mwishoni mwa ligi.

“Sio rahisi lakini tulichopanga kwetu sare ni haramu, ni bora tukapata ushindi wa bao moja, ambalo litatuongezea pointi tatu katika msimamo wa ligi.

“Hilo la mashabiki la kutaka soka safi, wasubirie kuona katika michezo ijayo ya ligi, ni baada ya katika mchezo dhidi ya Singida wachezaji wetu kuonesha mabadiliko ya kucheza soka la kuvutia,” alisema Ally.

SOMA NA HII  JEZI FEKI ZAIPA HARASA YANGA, MZIGO HUU UMEKAMATWA