Home news CHAMA, KAGERE NA MORRISON WAWALIZA MASHABIKI MBEYA…UONGOZI WATIA NGUMU …WADAI UTARATIBU…

CHAMA, KAGERE NA MORRISON WAWALIZA MASHABIKI MBEYA…UONGOZI WATIA NGUMU …WADAI UTARATIBU…


Pamoja na mzuka waliotua nao uwanja wa ndege wa Songwe, mashabiki wa Simba wameondoka kinyonge baada ya kutowaona nyota wa timu hiyo kufuatia kushindwa kufuata utaratibu wa mapokezi.

Ilikuwa hivi, baada ya mashabiki hao kuwasili uwanjani hapo walisubiri kwa takribani saa moja kufika kwa timu, ambapo makomandoo walikuwa makini kuweka utaratibu wa kuwapokea.

Wachezaji walipowasili wakiwa ndani ya uwanja wa ndege Songwe, mashabiki walianza kujaa mlangoni kwa ajili ya kuwaona nyota hao, jambo ambalo liliwafanya viongozi na makomandoo kuanza kuwapanga lakini walikwama.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu naye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwepo kutuliza fujo kwa mashabiki lakini haikuwezekana hadi kuamuliwa gari kuingia ndani kuwabeba wachezaji.

Kutokana na hali hiyo, wahudumu uwanjani hapo, waliamua kuruhusu gari la wachezaji na makocha kuingia ndani na kuwabeba huku mashabiki wakibaki wameduwaa wakisonya kutowaona wachezaji.

Mmoja wa mashabiki, Angelina Luhago amesema hajafurahia hali hiyo kwani ameacha shughuli nyingi lakini hakufikia malengo.

“Hapa nipo na familia yangu watoto wanne, wote tumekuja kuwaona wachezaji, tunasikia amekuja Chama, nilitaka nimuone, nimeumia sana” amesema Angelina.

Naye Faustina Job amesema amekereka na mashabiki ambao wameharibu utaratibu kwani kabla ya safari waliazimia kuwa na umoja na kufuata maelekezo ya viongozi.

“Siku nzima hatujala, tumeshinda na mambo ya timu, kwa ujumla nimeumia kutowaona wachezaji, kuna Kagere, Morrison na Chama ambaye tuna hamu sana kumuona” amesema Faustina.

Hata hivyo viongozi wa timu hiyo mkoani hapa hawakuonekana baada ya tukio hilo kuelezea kadhia hiyo.

SOMA NA HII  RASMI...MAYELE AKABIDHIWA DUME LA NG'OMBE NA SHABIKI WA MOROGORO ...LAFUGWA KLABUNI..