Home kimataifa MBAPPE AWACHANA MASTAA WENZAKE PSG KIMTINDO

MBAPPE AWACHANA MASTAA WENZAKE PSG KIMTINDO


STAA wa Paris Saint Germain,(PSG) Kylian Mbappe ameweka wazi kuwa wanatakiwa kufanya mambo ya pamoja na kushirikiana ili kuweza kufikia mafanikio lakini kama itakuwa tofauti na hivyo timu hiyo itakwama kufikia malengo hayo licha ya uwepo wa nyota wakubwa kama Lionel Messi na Neymar Jr.


Mbappe amesema kuwa yeye pamoja na Neymar Jr na Lionel Messi wakiwa mbele kwenye safu ya ushambuliaji ikiwa watashirikiana basi ana uhakika kwamba watafanya vizuri kwa msimu huu wa 2021/22.

Hivi karibuni Mbappe alionekana akimkosoa Neymar kutokana na kitendo cha yeye kushindwa kumpa pasi uwanjani jambo ambalo lilionekana kuwa gumzo kwa mastaa hao ghali wenye uwezo mkubwa wa kucheza na mpira namna ambavyo wanataka.

Kwa sasa timu ya PSG inatajwa kuwa ni timu yenye washambuliaji mahiri na uwezo mkubwa ila wamekuwa wakishindwa kuwa na ushirikiano mzuri jambo ambalo lilifanya iweze kupata kichapo cha mabao 2-0 dhidi ye Rennes kwenye mchezo wa Ligue 1 uliochezwa Oktoba 3.

“Pale unapocheza na wachezaji wa daraja la juu inahitajika kufanya vitu kwa kushirikiana ili muweze kufanya vitu kwa urahisi hutakiwi kusema kuwa mpe yule pasi yule usimpe,”. 
SOMA NA HII  STEPHANIE AWEKA REKODI MATATA KWA WAAMUZI