Home kimataifa OLE ANAPATA TABU KWELI NA REKODI ZAKE OLD TRAFFORD

OLE ANAPATA TABU KWELI NA REKODI ZAKE OLD TRAFFORD


 KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer kwa sasa anapambana kuweza kutatua tatizo la mwendo wa kutokuwa na mwendo mzuri ndani ya Uwanja wa Old Trafford kwa kuwa hajawa na mwendo mzuri. 

Mpaka sasa rekodi zinaonyesha kuwa ameweza kuongoza timu hiyo kwenye jumla ya mechi 53 ndani ya uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford jambo ambalo linawakera mashabiki.

Solskjaer ameanza kufanya hivyo kwenye mechi za hivi karibuni ambapo amekuwa akimpa nafasi ya kupumzika kwenye mechi za hivi karibuni ili aweze kumpa muda wa kupumzika.

Ingizo hilo jipya kutoka ndani ya Juventus, Ronaldo mpaka sasa ni mabao matano ameifungia timu hiyo kwa msimu wa 2021/22.

Timu hiyo ambayo imeondolewa mapema kwenye orodha ya timu ambazo zinaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 14.

Kwa msimu huu timu hiyo imeweza  kupoteza jumla ya mechi tatu ni kwenye mashindano yote iliyocheza.Ilianza kwa kunyooshwa na Young Boys kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kisha ikatolewa kwenye Carabao na West Ham United kisha ilipoteza mbele ya Aston Villa ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu England.

Rekodi za kocha huyo mpaka sasa zinaonyesha kuwa ameiongoza kwenye jumla ya mechi 53 aliweza kupata ushindi katika mechi 27.

Ni sare 15 alizikusanya, kichapo aliambulia kwenye mechi 11 akiwa amefungwa jumla ya mabao 63 na alishuhudia vijana wake wakifunga jumla ya mabao 107.

Ni mechi 14 alishuhudia wakikamilisha dakika 90 bila timu hiyo kufungwa yaani Clean Sheet ana wastani wa kupata ushindi asilimia 50.9 na ana wastani wa kupoteza kwa asilimia 20.8.

Pia kocha huyo kwa sasa anapambana kuweka usawa ndani ya kikosi hicho akitaka kuona kinafanya vizuri bila ya kumtegemea Cristiano Ronaldo.

SOMA NA HII  WAKATI KIVUMBI CHA QATAR KIKIENDELEA TENA LEO...ZINGATIA ODDS HIZI ZENYE UHAKIKA......