Home Habari za michezo SIMBA NA YANGA ZAFANYA KUFURU…ZIMEVUNA MAMILIONI HAYA KWA DK 90 TU

SIMBA NA YANGA ZAFANYA KUFURU…ZIMEVUNA MAMILIONI HAYA KWA DK 90 TU

IMEVUJA RASMI...KIPA KINDA SIMBA AWEKEWA ULINZI MZITO...ISHU KAMILI A-Z HII HAPA

Taarifa kutoka TFF imeeleza kuwa, mchezo wa dabi ya Simba SC dhidi ya Yanga SC imeingiza mapato ya shilingi Mil. 410,645,000.

Katika mchezo huo, jumla ya mashabiki 53,569 waliingia ambapo VIP waliingia watazamaji 340 kwa kiingillio ch shilingi 30,000 na kupatikana jumla y ash 10,200,000, VIP B waliingia watazamaji 4160 kwa kiingilio cha shilingi 20,000 ikapatikana jumla ya sh 83,200,000.

VIP C waliingia watazamaji 2,004 kwa kiingilio cha sh. 15,000 na kupatikana sh. 30,060,000 wakati jukwaa la rangi ya machungwa waliingia watazamaji 10,372 kwa kiingilio cha sh 10,000 na kupatikana sh. 103,720,000 na jukwaa la mzunguko waliingia watazamaji 36,693 kwa kiingilio cha 5000 na kupatikana sh 183,465,000.

TFF imetoa mgawanyo wa mapato hayo ambapo timu mwenyeji imepata sh 188,987,181.10 huku fedha zingine zikienda kwenye kodi, BMT na vitu vingine.

SOMA NA HII  JE SAMSUNG NA OPPO WATAWEZA KUJIBU MASHAMBULIZI HAYA YA Infinix NOTE 12 VIP KIRAHISI...?