Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO….NABI ASHTUKIA JAMBO ZITO YANGA….KAMBI YA AZAM YACHUNGUZWA KIJASUSI…

KUELEKEA MECHI YA KESHO….NABI ASHTUKIA JAMBO ZITO YANGA….KAMBI YA AZAM YACHUNGUZWA KIJASUSI…


WAKATI zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya Dabi ya Dar es Salaam ipigwe, Kocha Mkuu wa Yanga Mtunisia Nasreddine Nabi ameshitukia mitego ya wapinzani wao Azam FC na kuifyatua.

Dabi hiyo ya Dar es Salaam inayotarajiwa kuwakutanisha Yanga dhidi ya Azam inatarajiwa kupigwa Septemba 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zote mbili hivi sasa zipo kambini, Yanga ikiwa Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar huku Azam wenyewe wakijificha Azam Complex, Chamazi.

Kwa mujibu wa taarifa zinasema kuwa Nabi anatumia muda na akili nyingi kuiandaa timu yake ili ipate matokeo mazuri mara watakopovaana.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kocha huyo tayari amezipata mbinu zinazofanywa na wapinzani wake huko kambini ambazo ni kutumia kujaza viungo wengi kwa lengo la kutawala safu ya kiungo katika mchezo huo.

Aliongeza kuwa baada ya kufanya umafia huo na kugundua mipango hiyo, haraka ameanza kukiboresha kikosi chake kwa kukifanyia maboresho safu ya kiungo inayoongozwa na Stephane Aziz Ki, Khalid Aucho, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ na Feisal Salim ‘Fei Toto’ ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ya ushindi.

“Kwa muda mrefu Nabi amekuwa akiifutilia kwa karibu Azam, na kikubwa anataka kupata ushindi ili aendelee na rekodi yake ya msimu uliopita ya kutokufungwa.

“Hivyo alianza kuifuatilia tangu timu hiyo ilipokwenda Zanzibar kucheza mchezo wa kirafiki na haikutosha akawaomba viongozi wamtamfutie video mbili za michezo yao ya ligi ambayo ameicheza na uzuri ni kwamba amaezipata na kuzitazama.

“Haikutosha sasa amemtuma shushushu mmoja kwa ajili ya kwenda kufuatilia mazoezi ya Azam na kugundua mipango yao ya kutumia viungo wengi katika safu ya kiungo kwa lengo la kutaka kutudhibiti kutokana na ubora wetu uliokuwepo katikati, hivyo kocha ameliona hilo na haraka amebadili mbinu za uchezaji za kushambulia kutokea pembeni,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  NDEGE MPYA YA AZAM FC INAYOTEMBEA ARDHINI KUPITA KWA MWENDO WA TARATIBU