Kocha wa makipa wa Azam FC, Dani Cadena amesema atakaachini na kuzungumza na kiungo, Sospeter Bajana baada ya kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ulioisha kwa kufungana mabao 2-2.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Bajana alitolewa ilinafasi yake kuchukuliwa na Cleophance Mkandala jambo ambalo nyota huyo alionyweshwa kutokubaliana na mabadiliko hayo na kutoka moja kwa moja kwenda vyumbani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya mechi hiyo, Cadena alisema hakufurahishwa na kitendo alichio fanya Bajana kwani kimeonyesha taswira mbaya kitu ambacho atakaa naye ili kuzungumza ni kitu gani ambacho kilimpelekea kufanya maamuzi yale.
“Nadhani alitamani kuendelea na mchezo kwa sababu kabla ya hapo alicheza vizuri na hata ukiangalia vizuri tayari inaonyesha wazi tempa ilishampanda ndio maana ikatokea vile japo siwezi kuzungumzia kwa sababu nitaongea naye,”
“Kwa liwango chake kiujumla amecheza vizuri japo nimefurahishwa na wachezaji wote kwa jinsi walipambana kuanzia mwanzo, hii ndio mentality (mawazo) amabayo tunaijenga kwao ya kuhakikisha viwango vyao vinazidi kuimkarika.”
Cadena ndiye aliye simamia timu hiyo kwenye mchezo huo baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Abdihamid Moallin kupangiwa majukumu mengine huku Mfaransa, Denis Lavagne aliyetua juzi kwa ajili ya kuchukua mikoba hiyo akiwa jukwaani.