Home Habari za michezo BAADA YA ONYANGO KUUNGANA NA WENZAKE LEO…MGUNDA ASHINDWA KUJIZUIA…AANIKA MSIMAMO WAKE…

BAADA YA ONYANGO KUUNGANA NA WENZAKE LEO…MGUNDA ASHINDWA KUJIZUIA…AANIKA MSIMAMO WAKE…


Beki kisiki wa Simba SC, Joash Onyango, amerejea kwenye kikosi hicho baada ya kutoonekana tangu Msimu wa Ligi Kuu wa 2022-23 ulipoanza.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar leo Septemba 13, 2022 wakiwa tayari kwa safari ya kwenda jijini Mbeya kuwavaa Tanzania Prison, Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda amesema nyota huyo ameungana na wenzake tayari kwa safari.

โ€œYes Joash ameungana na wenzake na tutakuwa naye kwenye safari hii ya kwenda Mbeya kuwakabili Tanzania Prisons,โ€ alisema Mgunda.

Mbali na Onyango ambaye alipeleka maombi ya kuvunja mkataba wake na Simba TFF kisha taarifa zikieleza kuwa hakuruhusiwa, Mgunda alisema nyote wengine wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kupigwa kesho Septemba 14 katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.

โ€œKapombe ambaye alitoka kwenye majeruhi anaendelea vizuri hivyo wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa Kanoute ambaye ana kadi tatu za njano lakini pia anaumwa jino,โ€ alisema Mgunda.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPEWA MSAMAHA NA KUACHILIWA ...MWAKALEBELA AIBUKA NA JIPYA KUHUSU TFF NA YANGA....