Home Azam FC KUELEKEA MECHI YA CAF…KOCHA MFARANSA AWAPA MASHARTI HAYA AZAM FC…WAKISHINDWA IMEKULA KWAO…

KUELEKEA MECHI YA CAF…KOCHA MFARANSA AWAPA MASHARTI HAYA AZAM FC…WAKISHINDWA IMEKULA KWAO…


Kocha mpya wa Azam FC, Denis Lavagne juzi aliiongoza timu hiyo kwenye Ligi Kuu, ugenini dhidi ya Mbeya City, lakini tayari ameshaanza mikakati ya kuhakikisha inafanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika kuhakikisha Azam FC inatimiza lengo lake la kucheza kwa mara ya kwanza hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika kwa kufuzu mwaka huu, Lavagne ameutaka uongozi wa timu hiyo kuhakikisha anapata mikanda miwili ya video za mechi baina ya Al Akhidar ya Libya na Al Ahli Khartoum ya Sudan ambayo mojawapo watakutana nayo katika raundi ya pili ya michuano hiyo.

Tofauti na makocha wengine ambao hutuma baadhi ya maofisa wa benchi la ufundi au huenda wenyewe kutazama mechi baina ya timu husika ili waone moja kwa moja upungufu na ubora wa wapinzani kimbinu na kiufundi, Lavagne yeye ametaka mikanda ya video tu akiamini inatosha kuandaa mkakati wa kuwamaliza Waarabu.

Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ alisema kuwa hilo ni hitaji kubwa ambalo Lavagne ameanza nalo na uongozi wa timu hiyo utahakikisha unalitimiza.

“Kwa kweli malengo yetu siku zote ni kufanya vizuri katika mashindano ya klabu Afrika na ndio maana tumemleta kocha mwenye uzoefu na mafanikio makubwa katika soka la Afrika. Siku zote uongozi wa Azam FC umekuwa ukijipanga vizuri kuhakikisha hilo.”

SOMA NA HII  HARAKATI ZA USAJILI ZAANZA RASMI YANGA...NABI AKABIDHI MAJINA YA VYUMA 5 KWA HERSI...