Home Habari za michezo ACHANA NA RONALDO…HUYU HAPA STAA MWINGINE WA MAN UTD AMBAYE YUKO TOKA...

ACHANA NA RONALDO…HUYU HAPA STAA MWINGINE WA MAN UTD AMBAYE YUKO TOKA ENZI ZA FERGUSON…ANA ‘KIZIZI’ ..


Naweza kuamini kwamba kuna watu duniani wanaishi kwa janja janja , na wanaweza kupata kipato bila kufanya kazi.

Pale katika viunga vya Old Trafford Ä·una huyu bwana mdogo anaitwa Philip Anthony Jones ambae ni kiraka wa kuhudumu nafasi kama tatu kwa uwezo wake.

Philip Jones alijiunga na Manchester 2010 akitokea katika klabu ya Blackburn Rovers kwa ada inayotajwa kufika Pauni milioni 16.5, kwa wakati huo Man United ikiwa chini ya Kocha Sir Alex Ferguson.

Ikiwa ni miaka 12 sasa tangu kitasa huyu kujiunga na Mashetani Wekundu, amecheza michezo 229 na kufunga Magoli 6.

Jones ni Mwanaume ambaye amenusurika kuuzwa na Ferguson, Moyes, Louis Van Gaal, Giggs, Mourinho, Ole, Carrick, Ralf na bado anaishi hadi leo bila kupata nafasi ya kucheza.

Kitu cha kufurahisha na cha kuhuzunisha amekua Kila kikifika kipindi cha usajili wamekua anaumia.

Ukumbusho kwamba anapokea pauni milioni 4.5 kwa mwaka kutoka kwa Manchester United bila kufanya lolote.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KUKIWASHA KWENYE SIMBA DAY....ONANA AJA NA TAMBO ZA 'KIMWAKINYO'....