Home Habari za michezo ISHU YA KISINDA NA YANGA YAMUIBUA MAYELE PIA…AKUMBUSHIA MAMBO YA AS VITA...

ISHU YA KISINDA NA YANGA YAMUIBUA MAYELE PIA…AKUMBUSHIA MAMBO YA AS VITA …


Kisinda kaja? Nitafunga sana. Hivyo ndivyo alivyoanza kusema straika wa mabao wa Yanga, Fiston Mayele akizungumzia juu ya usajili wa nyota mpya wa timu hiyo, winga Tuisila Kisinda.

Mayele ameweka wazi kuwa amefurahishwa na ujio wa winga huyo ndani ya Yanga kutokana na uwezo wake wa kutengeneza mashambulizi kupitia pembeni.

Kabla ya wawili hao kukutana ndani ya Yanga msimu huu walishawahi kuchea pamoja kwenye kikosi cha AS Vita ya DR Congo chini ya kocha Florent Ibenge na kutwaa baadhi ya mataji likiwemo la ubingwa wa nchi hilo.

Mayele alisema kuwa ujio wa Kisinda kwake ni furaha kwa kuwa wamewahi kucheza wote na anafahamu ubora wa winga huyo haswa katika uwezo wake wa kupandisha mashambulizi kwa kasi kubwa jambo ambalo ni faida kubwa kwao washambuliaji.

“Kisinda ni mchezaji mzuri na tumewahi kucheza kwa pamoja wote AS Vita, nafahamu uwezo wake hivyo nafurahia kumuona amerejea tena ndani ya Yanga.

“Kile ambacho ni kizuri kwetu haswa katika safu ya ushambuliaji tunahitaji kupata nafasi nyingi, tunahitaji wachezaji wenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na naona kabisa Kisinda akija kutusaidia katika hilo kwa kuwa ni mchezaji mwenye kasi kubwa na mwenye kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga,” alisema Mayele.

Straika huyo ndiye kinara wa mabao ndani ya Yanga msimu huu akiwa ametupia mabao mawili ambapo msimu uliopita aliweka kambani mabao 16.

SOMA NA HII  IANZE WIKI YAKO KWA KUSHINDA MTINYO KIULAIINI KUPITIA CASINO YA KENO NDANI YA MERIDIABET..