Home Habari za michezo PAMOJA NA SIMBA KUPATA USHINDI UGENINI…KUMBE JUMA MGUNDA ALIFANYA KAZI HII YA...

PAMOJA NA SIMBA KUPATA USHINDI UGENINI…KUMBE JUMA MGUNDA ALIFANYA KAZI HII YA ZIADA KWENYE BENCHI…


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema aliwaambia wachezaji wacheze mpira jambo lililowapa matokeo chanya.

Jana, Simba ikiwa ugenini iliambulia ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa dakika 90.

Mabao ya Moses Phiri dakika ya 28 na John Bocco dakika ya 81 yalitosha kuipa ushindi timu ya Simba kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mgunda amesema kuwa aliwaambia wachezaji wapambane kwenye kusaka ushindi jambo hilo lilifanikiwa kwa kuwa walishinda.

“Ulikuwa ni mchezo muhimu kwetu kushinda na kila mchezaji alikuwa anapenda kuona matokeo yanapatikana na mwisho imekuwa hivyo.

“Niliwaambia wachezaji wacheze mpira kwa kushirikiana na kila mmoja alielewa na imekuwa hivyo, pongezi kubwa kwa kazi ambayo wamefanya lakini kazi bado haijaisha kuna mchezo mwingine mgumu unakuja,” amesema.

Mchezo ujao wa mkondo wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo mshindi wa jumla atajihakikishia nafasi ya kusonga hatua ya kwanza kimataifa.

SOMA NA HII  SIMBA MSIMU HUU HAITAKI KUFUNGWA, VIONGOZI WAJA NA HILI