Home Habari za michezo WAKATI SAKATA LA KISINDA HALIJATULIA…MAKAMBO NA MOLOKO WAWEKWA KWENYE MSITARI WA HATARI...

WAKATI SAKATA LA KISINDA HALIJATULIA…MAKAMBO NA MOLOKO WAWEKWA KWENYE MSITARI WA HATARI YANGA…


Mastaa wa Yanga, Heritier Makambo na Jesus Moloko licha ya kuponea tundu la sindano kung’olewa kikosini, wanakabiliwa na mtihani kujihakikishia usalama wa maisha Jangwani.

Licha ya Kocha Nasreddine Nabi kutokuwa na matumizi na Lazarous Kambole aliyejiunga msimu huu akitokea Kaizer Chief ya Afrika Kusini na Yacouba Sogne, lakini wanaendelea kufanya mazoezi na timu na wanaweza wakapindua meza muda wowote.

Makambo na Moloko wakilegeza kamba itawapa mpenyo Yacouba na Kambole kuingia kikosini kupitia dirisha dogo

Kitendo cha Yanga kuwaacha Kambole na Yacouba kikosini kimetafsiriwa kama kuwafanya Makambo na Moloko wajitume na kujua wakiteleza tu inakula kwao.

Beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa alisema: “Kama wanafanya mazoezi na timu hiyo, basi Moloko na Makambo watatakiwa kujituma ili kuonyesha hawajabakizwa kwa bahati mbaya, ukiachana na hilo kwenye nafasi ya Mokolo ameletewa Tuisila Kisinda na yupo Bernard Morrison, hiyo inaonyesha namna alivyo na kazi ngumu,” alisema.

Naye Edibily Lunyamila alisema kama Moloko ataendelea kuonyesha makali aliyoanza nayo atakuwa salama na atafanya makubwa kushangaza msimu huu.

“Yanga msimu huu inaonekana inahitaji kitu cha tofauti ndio maana kila nafasi ina ushindani, hata hao waliobakia wanafanya mazoezi inasaidia wachezaji wengine wasijisahau,” alisema.

Beki wa zamani wa timu hiyo, Bakari Malima alisema: “Kama wamebaki basi naona viongozi wana mpango mzuri wa kusuka Yanga itakayofanya makubwa kwenye Ligi Kuu na CAF,” alisema.

SOMA NA HII  MAYELE AWEKA REKODI HII MPYA...KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA