Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI ZA CAF…SIMBA SC WAANZA UMAFIA MAPEMA….WATUMA JESHI LA ‘VIWAVI’ LILONGWE...

KUELEKEA MECHI ZA CAF…SIMBA SC WAANZA UMAFIA MAPEMA….WATUMA JESHI LA ‘VIWAVI’ LILONGWE MALAWI…


Simba wako Dar es Salaam kimwili lakini akili na mipango yao yote ipo Lilongwe Malawi.

Katika kuhakikisha wanaanza kwa umakini kabisa kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets jana Jumanne kuna msafara wa watu maalumu watatangulia Malawi kwa ajili ya kuweka mazingira sawa.

Msafara huo wa watu maalumu utakwenda kuhakikisha mazingira na vitu muhimu vya ndani ya nje ya uwanja kabla ya timu kufika Alhamisi vinakuwa kwenye mpangilio mzuri na kuepuka fedheha yoyote kutoka kwa wageni ambao wameahirishiwa mechi zao mbili za Ligi ili kujiandaa kikamilifu.

Simba itacheza mechi ya kwanza ya hatua ya awali ugenini Jumamosi ya Septemba 10 kabla ya kurudiana nao Uwanja wa Benjamin Mkapa maarufu kama machinjioni Septemba 17

SOMA NA HII  KWA NINI YANGA WANAPATIA KWENYE USAJILI...? ENG HERSI KAFUNGUKA SIRI HII...