Home Makala ACHANA NA MESSI NA RONALDO…HUYU DOGO NDIYE MWANASOKA TAJIRI ZAIDI DUNIANI….ALAFU HANA...

ACHANA NA MESSI NA RONALDO…HUYU DOGO NDIYE MWANASOKA TAJIRI ZAIDI DUNIANI….ALAFU HANA ‘DEMU’ ETI…

[the_ad id="25893"]

Kama unaamini Christiano Ronaldo au Lionel Messi ndio wachezaji matajiri duniani basi unajidanganya hao wote wanatuliza kitenesi mbele ya huyu dogo ninayekwenda kukutajia.

Anaitwa Faiq Bolkiah mwenye miaka 24 akizaliwa 9 may 1998 Los Angeles Marekani. Faiq ni mtoto wa prince Jefri Bolkiah ambaye ni mdogo wake na Hassanal Bolkiah Sultan wa Brunei.

Anatajwa ndiye mcheza soka tajiri zaidi ulimwengu akimiliki utajiri wa dola za kimarekani billion 20 mbele ya Ronaldo mwenye utajiri wa dola milioni 460 na Messi mwenye utajiri wa dola milioni 400.

Faiq amecheza vilabu kadhaa vya uingereza kama vile Southampton, Chelsea na Leicester City, kwa sasa anacheza soka nchini kwao Brunei kwenye club ya Chonburi akiwa pia ni nahodha kwenye timu ya taifa.

Unaambiwa utajiri alionao Faiq anaweza kuwalipa mshahara mara 10 Ronaldo,Messi na Mbappe kwa wakati mmoja. Ameamua kucheza soka kama ni mchezo tu aupendao tokea akiwa mtoto mdogo kibongobongo tunaweza kusema “anajifurahisha”.

Faiq anamiliki gari 2300 kwenye garage yake, ndinga za gharama zote unazozijua wewe zisizo na idadi. Ana jumba ambalo hata yeye mwenyewe akisema alikague lote itamchukua hata miezi miwili.

Faiq alipotimiza miaka 7 baba yake prince Jefri alimualika Michael Jackson aje kutumbuiza kwenye party hiyo iliyohudhuriwa na wageni 3000 na alimlipa dola milioni 16 party iliyogharimu dola milioni 27 kwa ujumla na ilidumu kwa wiki mbili.

Faiq yupo single mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 24 na haijulikani kama aliwahi kudate na mwanamke yoyote maisha yake ya kimapenzi ni siri sana tofauti na baba yake na baba yake mkubwa ambao wana utitiri wa wanawake.

Pamoja na baba yake Faiq kuwa na wanawake wengi lakini mama yake na Faiq hajulikani wala hajawai kutajwa popote, wengine wanasema ni mmarekani wengine wanasema ni mmoja wa wake wa zamani wa prince Jefri ila hakuna anayemjua.

Faiq ana uraia wa nchi mbili marekani alipozaliwa na nchi ya asili yake Brunei.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here