Home Habari za michezo DIARRA AANZA ‘KUPOKOLEWA MAWE’ YANGA….MAKOSA YAKE YAIPONZA TIMU…

DIARRA AANZA ‘KUPOKOLEWA MAWE’ YANGA….MAKOSA YAKE YAIPONZA TIMU…

Tetesi za Usajili Yanga leo

KITENDO cha kipa wa Yanga, Diarra Djigui kuruhusu mabao matano katika mechi tano alizocheza kumewaibua mafaza kumchambua namna anavyoruhusu nyavu zake kutikiswa.

Diarra alikuwa kipa bora msimu uliopita lakini msimu huu ameanza vibaya baada ya mechi nne kuruhusu mabao matano kati ya mechi tano alizocheza kabla ya mchezo wa jana dhidi ya KMC.

Kipa huyo aliruhusu bao mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliomalizika kwa sare 1-1, Yanga 2-2, Ruvu Shooting 1-2 na 1-1 dhidi ya Simba.

Diarra mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Yanga ilishinda 3-0 kipa huyo alitoka baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika na kuingia Abuutwalib Mshery.

Upande wa Mshery amecheza mechi moja dhidi ya Coastal ambayo na walishinda 2-0.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Herry Morris alisema Diarra ana makosa madogo madogo na muda mwingine anaonyesha kuridhika jambo ambalo anatakiwa kuliacha.

“Kubadilika kwa safu ya ulinzi kwamba leo kacheza Job (Dickson) na Mwamnyeto (Bakari) kesho Bangala (Yanick) sio ishu sana kwa sababu hata msimu uliopita ilikuwa hivyo hivyo,” alisema Morris ambaye alisaini Yanga akitokea Prisons.

Kocha wa makipa wa Ihefu FC, Patrick Mwangata alimsifu Diarra kuwa na ubora kutokana na kupita katika misingi mingi lakini kwenye suala la uso kwa uso na washambuliaji sio mzuri.

“Kila kitu yupo vizuri hakuna ubishi, upande wa kucheza mashuti na kukutana uso kwa uso na washambuliaji kuna shida, nadhani akifanyia kazi mazoezini atakuwa bora zaidi,” alisema Mwangata.

SOMA NA HII  HUU NDIO UMAFIA WALIOUFANYA YANGA DHIDI YA SIMBA KWA MUSONDA...PICHA LILIANZIA HAPA..