Home Azam FC MAKOCHA ZAIDI YA 100 WAITAKA AZAM FC…..ISHU YA NABI KUTUA CHAMAZI YAIBUKA...

MAKOCHA ZAIDI YA 100 WAITAKA AZAM FC…..ISHU YA NABI KUTUA CHAMAZI YAIBUKA UPYA…

Habari za Azam FC

Baada ya kutimuliwa kwa kocha Mkuu wa kikosi cha Azam FC, Denis Lavagne, Uongozi wa klabu hiyo umepokea zaidi ya maombi 100 ya makocha wanaotaka nafasi hiyo.

Lavagne raia wa Ufaransa ambaye alijiunga na kikosi cha Azam hivi karibuni alisimamia timu hiyo katika michezo sita na kufanikiwa kushinda mechi tatu na kupoteza tatu.

Akizungumzia mchakato wa kumpata kocha Mkuu, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe alisema tayari wameanza kupokea maombi ya makocha mbalimbali wakihitaji kukinoa kikosi chao.

“Tunamshukuru Mungu kikosi kipo salama chini ya Kaimu kocha Mkuu, Kali Ongala.

“Tumepokea CV za makocha mbalimbali ambao ni zaidi ya 100 kutoka ndani na nje ya Tanzania wakihitaji kufanya kazi ya kukinoa kikosi chetu.

“Uongozi unaendelea kuyafanyia kazi na mchakato ukikamilika basi kocha atatangazwa. Hakuna asiyetamani kufanya kazi na kocha kariba ya Nabi lakini tunamheshimu kwani yupo kwenye timu nyingine.”

SOMA NA HII  KISA YANGA KUFUNGWA...KAMWE AWASHUKIA WAANDISHI WA HABARI KWA KUIPENDELEA IHEFU...