Home Habari za michezo WAKATI YANGA WAKIENDA SUDAN LEO….HIZI HAPA SABABU ZA SURE BOY KUPIGWA CHINI...

WAKATI YANGA WAKIENDA SUDAN LEO….HIZI HAPA SABABU ZA SURE BOY KUPIGWA CHINI MAZIMA…

Yanga imewaweka hadharani wachezaji 25 wanaowafuata Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika huku kiungo fundi Salum Aboubakar’Sure boy’ na winga Kinda Denis Nkane wakiachwa.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba Sure boy ataikosa safari hiyo kuelekea mchezo wa Jumapili Oktoba 16 dhidi ya Al Hilal kufuatia kuugua Malaria na homa ya matumbo huku Nkane akiwa na shida katika pasi yake ya kusafiria.

Baada ya sare ya bao 1-1 nyumbani, Yanga itahitaji ushindi wowote au sare ya kuanzia mabao mawili kusonga mbele kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Katika orodha hiyo Yanga itaondoka na makipa watatu Diarra Djigui, Aboutwalib Mshery na Erick Johola. Mabeki wako 8 wakiongozwa na nahodha mkuu Bakari Mwamnyeto,Yannick Bangala, Dickson Job,Kibwana Shomari,Djuma Walo, Mutambala Lomalisa,Ibrahim Abdulla ‘Bacca’,David Brayson.

Kuna viungo 9 ambao ni Feisal Salum, Khalid Aucho,Gael Bigirimana,Zawadi Mauya,Farid Mussa, Dickson Ambundo, Jesus Moloko,Twisila Kisinda na Bernard Morrison. Washambuliaji wako 5 Stephane Azizi KI, Yusuf Athuman,Clement Mziza, Heritier Makambo na mfungaji wao tegemeo Fiston Mayele.

Yanga imeondoka leo kwa Ndege ya shirika la Ethiopia wakipitia jijini Addis Ababa nchini humo kabla ya kuunganisha nchini Sudan tayari kwa mchezo huo utakaoanza majira ya saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE - KITUO KINACHOFUATA KWA SIMBA NI KWA WAKUBWA WENZAO...TUTAONA UKUBWA WAO..