Home Habari za michezo UINGEREZA ‘WAUA MENDE KWA RUNGU’…SENEGAL BILA YA MANE YAKUNG’UTWA…

UINGEREZA ‘WAUA MENDE KWA RUNGU’…SENEGAL BILA YA MANE YAKUNG’UTWA…

Mabao 8 yamepatikana kwenye mchezo wa Kombe la Dunia huko Qatar baada ya dakika 90 kukamilika kati ya England dhidi ya Iran.

Ubao wa Uwanja wa taifa wa Khalifa umesoma England 6-2 Iran kwenye mchezo wa kundi B.

Mabao ya Jude Bellingham dakika ya 35, Bukayo Saka dakika ya 43 na 62, Raheem Sterling dakika ya 45+1, Marcus Rashford dakika ya 71 na msumari wa mwisho ulipigwa na Jack Grealish dakika ya 89.

Msumari wa Grealish ulikamilisha idadi ya mabao 6 huku yale mawili kwa Iran yakifungwa na Mehdi Tarem dakika ya 65 na 90+13 kwa mkwaju wa penalti.

Aidha katika mchezo mwigine, Uholanzi ilifanikiwa kuibuka naushindi dhidi ya Senegal.

SOMA NA HII  WAKATI ISHU YA CHAMA NA PHIRI IKIWA HEWANI BADO...PABLO AMALIZA KILA KITU SIMBA..MAGORI ATEMA CHECHE..